TARURA YAWAKANA WANANCHI WALIBOMOA KUTA ZA NYUMBA100 ZA WENZAO ,WATAKIWA KUADHIBIWA ,WALIDAI WAMETUMWA NA TARURA KUPANUA BARABARA,YAWATAKA KUFUATA SHERIA!

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


SAKATA la wakazi wa kitongoji cha Olisiva  kata ya Olorien wilayani Arumeru,kubomolewa kuta za Nyumba zao zaidi ya 100  na wananchi wenzao wakishirikiana na viongozi wa kata kwa madai ya kutengeneza barabara, limechukua sura mpya.

Aprili 12 Mwaka huu,wananchi zaidi ya 200  wa kata hiyo ya Olisiva waliendesha bomoabomoa ya kuta za nyumba kwa madai ya kupanua barabara na kufanya uharibifu mkubwa wa mali za watu ambao  wakidai hawakushirikishwa juu ya uwepo wa mpango huo.

Wakitoa malalamiko yao wakazi hao walimtuhumu mwenyekiti wa kitongoji cha Olisiva,Loshie Jonasi,diwani wa kata hiyo, Erick Samboja na afisa mtendaji wa kata hiyo, Charles Sikoy kuongoza bomoabomoa hiyo haramu ambao waliokuwa wakiwahamasisha wananchi kubomoa kuta zinazoonekana kuwa ndani ya eneo la barabara.


Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake mapema leo Aprili 15,2025,meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Mkoa wa Arusha, mhandisi Nicolaus Francis alisema Tarura haihusiki na mpango huo na wala haikuwatuma watu hao kujichukulia sheria mkononi na kubomoa kuta za nyumba za watu bali ni wahalifu kama wahalifu wengine na wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Tarura inataratibu zake na pale tunapohitaji kufanya upanuzi wa barabara lazima tuwashirikishe wananchi na kuingiza mradi huo  kwenye bajeti ,kwa hiyo madai ya viongozi kuwa tuliwapatia baraka zote za kubomoa barabara  hiyo yenye urefu wa kilomita 0.6 ni uongo kwani hata hiyo barabara ya kanisani haipo kwenye mamlaka yetu"

Alisisitiza kuwa wananchi hao wako kinyume cha sheria na kuwataka iwapo wanataka kuongeza korido wanapaswa kuleta maombi iali Tarura waiweke kwenye mpango wa mwaka wa fedha na kwa mwaka huu wa fedha wa 2025/2026 barabara hiyo haiko kwenye mpango wao.

"Sisi Kama Tarura maamuzi ya vikao halali vya serikali za mitaa ama vijiji kupitia viongozi wao sisi huwa hatuwaingilii,lakini kama maamuzi yao hayakufuata vikao halali sheria itachukua mkondo wake na hao wananchi waliovunjiwa wakijiridhisha kama taratibu hazikufuatwa wanaweza kuchukua hatua"Alisema.

Kwa upande wa mwenyekiti wa kitongoji cha Olisiva Loishie Jonas alisema kuwa waliohusika na zoezi hilo la bomoabomoa ni wananchi na sio viongozi kama inavyodaiwa ila mazimio ya mkutano wa wananchi walioketi Machi 22,2025 na kuadhimia kupanua barabara hiyo.

Ends...







Post a Comment

0 Comments