HOSPITALI YA AGA KHAN KUMENUKA MTEJA AIDAI BILIONI 1.2 KWA KUSABABISHA MTOTO WAKE KUKATWA MGUU KWA UZEMBE,MAHAKAMA YASEMA KESI IPO KUUNGURUMA MWISHO WA MWEZI !

 Na Joseph Ngilisho -DAR ES SALAAM 


MKAZI wa Msongola wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, Ally Mkii amefungua mashtaka ya madai mahakamni dhidi ya hospitali ya Aga Khan iliyopo Jijini humo ,akitaka kumlipa kiasi cha  shilingi bilioni 1.2 kama fidia iliyotokana na uzembe wa hospitali hiyo na kusababisha  mtoto wake  kukatwa na kuondolewa kwa mguu wake wa kulia na hivyo kuwa na ulemavu wa kudumu.



Ally amefungua shauri hilo la madai namba 26889/2024,Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ndogo ya Dar es Salaam,chini ya jaji Hussen Salum Mtembwa akiwa na  madai kwamba  mtoto wake alifanyiwa uzembe wa kimatibabu na kusababisha kuondolewa kwa mguu wake uliokuwa umeumia kwa kujikwaa akiwa anacheza na wenzake.
Wakili Kurubone 

Wakili wa  utetezi wa upande wa mashtaka,Pasensa Kurubone alifafanua kwamba shauri hilo la madai limefunguliwa katika mahakama hiyo , ambapo washtakiwa ni hospitali hiyo pamoja na daktari aliyehusika na matibabu ya mtoto.

"Kimsingi shauri hili ni la madai dhidi ya hospitali hiyo pamoja na daktari mwajiriwa wa hospitali hiyo aliyesababisha madhara ya mtoto, na mteja wangu katika shauri hilo anasimama kama kimvuli cha mtoto aliyesababishiwa madhara na wakati yanafanyika alikuwa na umri wa miaka miwili na kwa mujibu wa kisheria hawezi kusimama mwenyewe mahakamani"

Alisema kuwa mteja wake anadai fidia ya unafuu iliyotokana na madhara yaliyopelekea mguu wa mtoto wake kukatwa na kutaka  kulipwa fidia ya unafuu kiasi cha sh,milioni 700,na sh, Milioni 500 kama nafuu za ujumla ikiwemo usumbufu .

Alisema baada ya kuwasilisha maombi yao ya fidia ,upande wa wadaiwa walileta pingamizi wakidai kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa sababu ni masuala ya kitabibu yanayopaswa kusikilizwa kwenye mabaraza ya wakunga.

Hata hivyo baada ya mapingamizi hayo, jaji Mtembwa wiki iliyopita alitoa uamuzi wa kutupilia mbali na kudai kuwa maombi ya walalamikaji yanamsimgi na hivyo kesi hiyo kupangwa kuendelea  Aprili 30 Mwaka huu itakapo kuja kwa ajili ya kutajwa ili kupanga namna ya uendeshaji wa shauri hilo.

Kwa upande wa Mlalamikaji Ally Mkii,baba mzazi wa mtoto, aliishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki baada ya kutupa mapingamizi ya upande wa utetezi na kuona kwamba ipo kesi ya msingi ya kusikilizwa.

Akisimulia mkasa wa mtoto wake,Mkii alisema kwamba mwaka 2022 mtoto wake akiwa anacheza na wenzake mtaani aliumia na kupelekwa katika hospitali hiyo ya Aga-khan katika tawi la Mbagala 

Alisema baada ya kufika mtoto wake alifanyiwa kipimo cha picha(Xray)na baadaye kuamuliwa kupelekwa katika hospitali kubwa iliyopo jijini Dar ambapo  alifanyiwa kipimo na kugundulika kuwa mguu umevunjika na kufungwa POP.

Alisema alirejea nyumbani akiwa na mtoto na ndani ya siku nne aliona maendeleo ya mtoto sio mazuri na kuamua kumrejesha tena katika hospitali hiyo na baada ya kufika  alifanyiwa kipimo cha CT scan na ultrasound na kugundulika kuwa damu haitembei kwa sababu pop ilikuwa imebana, ilifungwa vibaya na kumshauri  mguu ukatwe.

"Sikukubaliana na hilo niliomba niende hospitali kubwa ya Taifa Muhimbili na nilipofika waligundua kuwa damu haitembei na kushauri pia mguu ukatwe haraka na ukicheleweshwa mtoto anaweza kupoteza maisha ,nilikubaliana na mguu kukatwa ili kunusuru maisha yake"

Alisema baada ya hapo aliamua kuandika barua kwa hospitali ya Agakhan kuomba msaada wa gharama za matibabu  baada ya wao kusababisha uzembe wa mtoto wake .

"Barua yangu haikujibiwa niliamua kwenda kwa waziri Ummi Mwalimu na kumweleza aliamua kuinda timu ya wizara walinihoji na baadaye kukawa na ukimya wa muda mrefu sana na nilipokuwa nikifuatilia waliniambia nisubiri majibu nanpia hata waziri aliacha kunipa ushirikiano"Alisema.


"Baada ya ukimya wa muda mrefu tangu mwaka 2022 ndio maana nimeona nikimbilie mahakamani kwa ajili ya kupata haki ya mtoto wangu ambaye amepata ulemavu wa kudumu kwa uzembe wa hospitali ya Agakhan"Alisema Mkii.

Ends...


Post a Comment

0 Comments