By Ngilisho Tv-VATCAN
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amefariki dunia leo Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88. Taarifa rasmi kutoka Vatican zinaeleza kuwa Papa Francis amefariki akiwa nyumbani kwake katika makazi ya Casa Santa Marta, Vatican.
Muda mfupi uliopita, Mwadhama, Kardinali Farrell, alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis, kwa maneno haya:
"Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa sina budi kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko,Saa 7:35 asubuhi ya leo (saa za huko), Askofu wa Roma, Francis, alirudi nyumbani kwa Baba. Maisha yake yote yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na Kanisa Lake."
Papa Francis, aliyezaliwa mwaka 1936, amehudumu kama Papa tangu mwaka 2013 na alikuwa kiongozi wa kwanza wa Kanisa Katoliki kutoka Amerika ya Kusini.
Mwaka 2013 Francis alikuwa Papa wa kwanza kutoka Amerika na kutoka Ulimwengu wa Kusini. Alimrithi Benedict XVI, ambaye alifariki mwaka 2022. Benedict XVI alikuwa Papa wa kwanza kustaafu kwa hiari baada ya takribani miaka 600.
Papa Francis jina lake kamili ni Jorge Mario Bergoglio, alikuwa Kardinali wa Argentina, na alikuwa na umri wa miaka sabini alipokuwa Papa mwaka 2013.
Bergoglio aliwavutia wahafidhina juu ya mtazamo wake kwa masuala ya mahusiano, huku akiwavutia wanamageuzi kwa msimamo wake wa kiliberali juu ya haki za kijamii.
Lakini ndani ya urasimu wa Vatikani baadhi ya majaribio ya Francis ya kuleta mageuzi yalikumbana na upinzani, lakini alibaki kuwa maarufu miongoni mwa wanamapokeo.
0 Comments