By ngilishonews.com
Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amehitimisha ziara yake kwa kukutana na Rais wa Burkina Faso, Mhe. Captain Ibrahim Traoré.
Mkutano huo ulifanyika jijini Ouagadougou Aprili 17, 2025 na kuhudhuriwa na maafisa waandamizi kutoka Serikali zote mbili. Katika mkutano huo, Mhe. Kikwete alielezea shukrani zake kwa kupata fursa ya kukutana na Captain Traoré na kumkabidhi ujumbe maalum wa Rais Samia.
"Rais wangu amenituma nije kuwasilisha Ujumbe Maalum kwako na nimefurahi umenipa fursa hiyo na leo umeupokea rasmi", Alisema Dkt. Kikwete.
Dkt. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia kuhusu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Afrika, hususan kubadilishana uzoefu ili kwa pamoja Afrika iweze kuendeleza rasilimali zake kwa faida ya watu wa bara lao.
0 Comments