HABARI KUU

6/recent/ticker-posts

MGOGORO NGORONGORO,SHIRIKA LAIANGULIA SERIKALI, LATAKA MASHIRIKA NA NGO'S CHONGANISHI YACHUKULIWE HATUA KALI, YANACHOCHEA MGOGORO ILI KUPATA FEDHA ZA WAFADHILI WATOTO NA WANAWAKE WAATHIRIKA NAMBA MOJA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Mimutie Women Organization la nchini Tanzania limeitaka serikali kukaa meza moja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, NGO's na wananchi waishio wilayani Ngorongoro ili kujadili mgogoro usiokoma wa mipaka ambao unaendelea kuwaumiza jamii ya kifugaji hasa wanawake na watoto.

Aidha shirika hilo limeiomba serikali kuchukua hatua kali kwa mashitaka ambayo yamekuwa yakichochea migogoro ya Ardhi wilayani humo na kuwachonganisha wananchi na serikali yao kuhakikisha mgogoro hiyo haikomi na wao kuendelea kujinufaisha na fedha wanazopata kutoka kwa wafadhili.

Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Mimutie Women Organization Rose Njilo alisema suala la migogoro ya Ardhi wilayani Ngorongoro limekuwa kikwazo cha maendeleo ya wananchi wa jamii ya kifugaji na limekuwa neema kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanaoutumia mgogoro huo kujinufaisha.

Alisema ipo haja kwa serikali kukutana na waathirika wa Migogoro hiyo ili kuwajengea uwezo na kuleta mahusiano mazuri kati yao na mamlaka za uhifadhi ili waweze kujua mipaka na kuiheshimu.

Mkurugenzi huyo alisema baadhi ya mashirika yamekuwa na ushawishi mkubwa kwa jamii za kifugaji na hivyo kuwajengea imani potofu wananchi ili waichukie serikali  ,wawekezaji pamoja na mamlaka za hifadhi.

Alisema shirika hilo limefanya utafiti na kuibaini kwamba migogoro hiyo ya Ardhi imekuwa na athari kubwa kwa wanawake na watoto na hivyo kuiomba serikali kukaa meza moja na makundi hayo ili kufikia mwafaka wa migogoro ya ardhi.

Kwa kutambua hayo shirika hilo la Mimutie Women Organization limeamua kutumia mkutano wa 77 wa tume ya kitaifa ya haki za kibinadau unaoendelea jijini hapa kupaza sauti zao na kulaani watu wachache walioigeuza migogoro ya Ngorongoro kama fursa ya kujiingizia kipato kutokana na fedha za wafadhili.

"Suala la Mgogoro wilaya ya Ngorongoro limekuwa na athari kubwa kwa makundi maalumu ,wanawake,watoto na vijana na baadhi wa watu wanatumia migogoro hiyo kama fursa ya kujipatia kipato"

Njilo aliiomba serikali kuangalia namna ya kukutana na jamii hiyo inayoteswa na migogoro isiyoisha ili kurudisha tumaini hususani kwa wanawake na watoto ambao wamekuwa wakiishi kwa mateso makubwa kutoka na mifugo yao kukamatwa na kutozwa faini kubwa.

Alifafanua kwamba septemba 19, 2023 mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Arusha ilitoa uamuzi katika shauri namba 21 la mwaka 2022 ambapo wananchi watano walifungua shauri mahakamani dhidi ya waziri wa maliasili na utalii na mwanasheria wa serikali wakipinga uamuzi wa kumegwa kwa eneo wanaloamini ni mali yao ili kuwa pori tengefu la Pololeti.

Alisema maamuzi ya mahakama chini ya Jaji Tiganga yaliamua kuwa eneo hilo litabaki kuwa eneo tengefu  kwa kuzingatia  masharti yote ya mapori tengefu yataendelea kufuatwa ikiwemo kutoingiza mifugo.

Alisema maamuzi hayo yalitafsiliwa vibaya na baadhi ya watu waliwachochea wananchi ambao walianza kuingiza mifugo yao kwenye eneo hilo na kujikuta mifugo yao ikikamatwa na kutozwa faini kubwa na hivyo baadhi yao kufilisika.


Ends. .












Post a Comment

0 Comments